Katika jitihada za kuhakikisha kwamba TABCO inafanyika kwenye ubora uliokusudiwa. Baadhi ya mashindano ya majaribio yamekuwa yakiandaliwa ikiwa ni kwa nia ya kujifunza changamoto mbalimbali kabla ya kufanya shindano kubwa zaidi. Shindano la kwanza la majaribio la Utangazaji na Uandishi wa Habari lililosimamiwa na timu ya TABCO lilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa nane (8) mwaka 2018 kwa kuchukua washiriki kutoka Chuo cha Uandishi wa Habari cha Dar es Salaam (DSJ). Shindano hilo lilikuwa na lengo la kuendeleza kukuza taaluma ya uandishi wa habari pamoja na kuinua vipaji vya wanafunzi katika kujifunza zaidi kwa mafunzo ya vitendo.

 

UENDESHAJI WA VIPINDI KATIKA MASHINDANO TABCO

Katika shindano hili kulikuwa na vipengele vinne (4), kama ifuatavyo :

1. Kusoma habari (News Bulletin)

2. Kipindi maalum (Special Program)

3. Michezo (Sports)

4. Burudani (Entertainment)

 

WAFUATAO NI MAJINA YA WASHINDI WA MASHINDANO HAYA

1. Jina Clement Robert ni mshindi wa kipindi maalum (Special Program) - DSJ

2. Jina Matilda Peter ni mshindi wa kipindi cha Burudani (Entertainment) - DSJ

3. Jina Florian Rutaihwa ni mshindi wa kipindi cha msomaji wa habari (News Bulletin) - DSJ

4. Jina Jabir Hamisi ni mshindi wa kipindi cha Michezo (Sports) - DSJ

 

WAFUATAO NI ORODHA YA MAJAJI WALIOFANIKISHA MASHINDANO HAYA

1. Jina la jaji Mkuu Grace Kingalame, Kutoka Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Mwandishi wa habari na mtangazaji/ Mjumbewa Baraza la UWT Taifa

2. Jina la jaji Ester Emandus Mwandishi wa habari Mtangazaji kutoka chombo cha habari Channel Ten

3. Jina la jaji Godwin Mawanja, Mwandishi na mtangazaji wa habari kutoka Chombo cha habari E-fm Radio na TV

4. Jina Frank Gibebe Mtangazaji na mwandishi kutoka chombo cha habari East Africa


Habari Mpya