Kuhusu TABCO
Tunafahamu kuwa soko la ajira nchini ni gumu, na mara nyingine inatokana na ukosefu wa ujuzi zaidi kutoka kwa muhusika kulingana na fani aliyosomea. Hivyo katika kukuza Tasnia ya Utangazaji wa Redio na Runinga tumekuletea mashindano wakati muafaka kwa ajili yako wewe kijana, ili kukupa ujuzi zaidi na hivyo kukuwezesha wewe mwenye kipaji lakini ukakosa fursa ya kukiendeleza ili uweze kujiajiri na pia kuajirika katika vyombo vya habari nchini na duniani kwa ujumla wake.
Tanzania Broadcasting Competition (TABCO) ni Shindano ya Utangazaji wa Redioni na Runingani lililoasisiwa mwaka 2015 na kusajiliwa rasmi BRELA mwaka 2018. Shindano hili linalenga kutoa maarifa na ujuzi zaidi juu ya namna bora ya kutangaza taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari nchini. Tunatambua una kipaji, lakini kipaji bila ujuzi hakiwezi kufanya kazi kwa weledi na ufanisi.
Hivyo basi, Union of Training Institution (UTI) ikishirikiana na wadau mbalimbali iliamua kuanzisha Shindano hili la Utangazaji wa Habari za Redioni na Runingani ili kutambua na kuinua kipaji chako na kukuongezea ujuzi utakaokufanya kuwa Mtangazaji bora na maarufu.
Shindano hili kuwa na zawadi lukuki kwa Washiriki, ikiwemo “scholarship”, pamoja na nafasi za ajira kwa wanaoibuka kuwa washindi. Kifanye kipaji chako kuwa ujuzi wako na hivyo kuwa ajira yako kwa kujiongezea kipato na kuleta maendeleo nchini.