MASHARTI NA VIGEZO VYA KUSHIRIKI TABCO
Ili uruhusiwe kushiriki shindano la TABCO unapaswa kuwa na vigezo vifuatavyo:
- Usiwe mfanyakazi wa DSJ wala Taasisi yoyote yenye uhusiano na DSJ
- Usiwe mwanafunzi wa Chuo chochote cha Uandishi wa Habari na Utangazaji
- Usiwe umesomea fani ya Uandishi wa Habari na/au Utangazaji katika ngazi yoyote
Endapo utabainika kukiuka vigezo na masharti haya:
- Utafunguliwa mashitaka kwenye Mahakama halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tuhuma za udanganyifu
- Endapo ulishinda, ushindi wako hautatambulika na hivyo utatakiwa kurudisha zawadi zote ikiwemo Ufadhili wa masomo na Cheti cha ushindi