Tarehe ya Chapisho 2018-06-17
Unataka kuwa Mtangazaji wa Redio na Runinga mwenye umaarufu na weledi unahotajika kwa waajiri nchini na hata nje ya nchi? Suluhisho pekee ni kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam(DSJ) ambapo pamoja na kujifunza kwa vitendo juu ya kurusha matangazo kwa njia ya Redio, Runinga na Mitandao, pia utapata fursa ya kushiriki katika mijadala ya kitaaluma na mashindano mbalimbali yatakayokufanya uweze kukidhi changamoto zilizopo katika ushindani wa soko la ajira.
Aliyasema hayo juzi, naibu mkurugenzi wa umoja wa taasisi za mafunzo (UTI), Geofrey Chami, alipokuwa akifungua siku ya mitandao ya kijamii duniani yaliyofanyika ndani ya majengo ya Baraza la Sanaa nchini (BASATA), aliongeza kuwa, tasnia ya habari nchini hukua siku hadi siku hivyo basi, sisi kama wadau hatuna budi kutumia mitandao ya kijamii kwa ufanisi na faida zaidi, mitandao isiwe ni sehemu ya kupenda picha au kutoa maoni juu ya picha au jambo fulani lililopo kwenye waraka wa mtu fulani.
“Ili tutambue kuwa una ujuzi wa kufanya jambo fulani, ni lazima udhihirishe kwa vitendo, vitendo vyako ndio kipimo tosha juu ya kutambua fani yako unaijua kwa kiwango gani”, alisema.
Katika jitihada za....
Chuo cha uandishi....
Unataka kuwa Mtangazaji wa Redio....