Tarehe ya Chapisho 2018-06-17
Chuo cha uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) kinakualika kushiriki katika mashindano yaurushaji wa matangazo kwa njia ya redio.
Mashindano haya yanalenga kuwaongezea ujuzi zaidi kwa wana habari wanaoibukia katika tasnia ya utangazaji na wale wenye vipaji ili kuweza kujiajiri na kuajirika kiurahisi katika vyombo vya habari nchini.
Jaochim Rupepo, mkuu wa Chuo hicho amesema, katika kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa, chuo kinafanya vizuri katika utoaji wa mafunzo ya uandishi wa habari na mawasiliano ya umma, tunameandaa mashindano yajulikanayo kama Tanzania Broadcasting Competition (TABCO) yaani mashindano ya utangazaji nchini, ambapo tutazunguka mikao mitano kutafuta washiriki. Alisema, mashindano haya yatawaonyesha wadau katika tasnia ya habari kuwa, pamoja na wahitimu tunaowatoa kila mwaka lakini pia mtaani kuna vipaji vingi ambavyo kwa pamoja tukiviendeleza tasnia ya habari nchini itakuwa kwa kasi zaidi. “Tumekuwa katika tasnia hii ya mafunzo ya uandishi wa habari na utangazaji takribani miaka ishirini, tuna uzoefu wa kutosha pia tunaamini mashindano haya yataleta mchango mkubwa katika nchi na kwa waandishi wanaoibukia.” azma yetu ni kufika mikoa yote nchini.”
Akitoa ufafanuzi namna ya kushiriki, alisema, jinsi ya kushiriki mashindano haya, tafadhali ingia katika kiunganishi cha www.tabco.co.tz, na hakuna vigezo na masharti magumu kujiunga na kushiriki.
Katika jitihada za....
Chuo cha uandishi....
Unataka kuwa Mtangazaji wa Redio....